Kyiv inasema inamzuilia mwanaume mwenye asili ya Ukraine anayefanya kazi ya kujitolea na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa kuwasaidia wanajeshi wa Urusi kuingia mashariki ya taifa hilo.
Kulingana na SBU, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 34 anayefanya kazi ya kujitolea na WFP, alikuwa na majukumu ya kutambua walipo wanajeshi wa Ukraine na vifaa vyao karibu na mji wa Pokrovsk, na kutoa taarifa kwa Urusi kutekeleza shambulio.
Imeripotiwa kuwa mshukiwa tayari anazuiliwa na kwamba anakabiliwa na tishio la kufungwa maisha jela kwa makosa ya uhaini mkubwa.