Jeshi la Polisi mkoani Njombe linamshikilia Castory Abusalam Kindole mwenye umri wa miaka 48 mkazi wa Kijiji cha Idindilimunyo wilayani Wanging’ombe kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Sifa Lusemwa (37) kwa wivu wa mapenzi.
Akithibitisha kushikiliwa mtuhumiwa huyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga amesema marehemu Sifa alikutwa ameuawa nyumbani kwake kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kufariki dunia.
Aidha Kamanda Banga ameongeza kusema kuwa sababu za kutokea kwa tukio hilo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kutoka nje ya ndoa kwa muda mrefu.