Jamaa Atumikia Kifungo cha Miaka 10 Jela Sababu ya 'Kumuambukiza' Mpenziwe Ukimwi

Mwanamume Mkenya ambaye amekuwa akitumikia kifungo cha miaka 10 jela amesimulia kuwa alimficha mpenzi wake kuhusu hali yake ya Ukimwi kwa sababu alikuwa na wasiwasi angemwacha.

Arthur Wachira, ambaye anatumikia kifungo chake katika Gereza la King'ong'o, alisimulia hali ya kutatanisha iliyompeleka jela. Ataachiliwa 2027 baada ya kumaliza kifungo chake. 

 mwanamume huyo alisema hakumwambia mpenzi wake kuwa ana VVU, na hivyo alipogundua alivunjika moyo sana. 

"Mimi nilikuwa mwendesha bodaboda, mahusiano yetu yalivyozidi kushamiri alihamia kwangu kwa sababu ya masuala yaliyokuwa yanamkabili nyumbani. Kuishi kwetu kulikuwa kwa utulivu kwa siku tano za mwanzo, lakini sikumweleza kuwa nina VVU. Nilidhani ataniacha ikiwa angejua," alisema. "Siku alipogundua, alipatana na dawa yangu, na aliumia moyoni na kudaiwa) alijiua," aliongeza. Wachira alidai kuwa alirejea kutoka kazini na kupata dawa zake za ARV zimetapakaa sakafuni baada ya mwanamke huyo kuzipata. Pia alidai aliupata mwili wake ndani ya nyumba. 


Nilikuta nyumba imefungwa kwa ndani, nikachungulia ndani ya nyumba na kuona maiti yake, nilichukua maiti yake na kutupa shambani, kisha nikajisalimisha kwa polisi na kukiri kumuua, sikujua. nini cha kufanya," aliongeza. Mwanamume huyo anasisitiza kuwa, hata hivyo, hakumuua mpenzi wake. “Najua hivi sasa iwapo ningepiga simu polisi nilipopata mabaki hayo, sitakuwa gerezani,” mfungwa huyo alisema. 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii