Maelfu ya nyumba yakumbwa na mafuriko Korea Kaskazini

Zaidi ya nyumba 4,000 katika mji wa Sinuna na eneo la Uiju lililoko karibu na mpaka wa China nchini Korea Kaskazini zimekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha katika maeneo hayo.


Haya yameripotiwa leo na shirika la habari la serikali KCNA.

KCNA imeripoti kuwa zaidi ya ekari 7,000 za mashamba pamoja na majengo kadhaa ya  umma na barabara pia zimekumbwa na mafuriko na kusababisha mkutano wa dharura wa siku mbili wa Kamati Kuu ya chama tawala cha Wafanyakazi mapema wiki hii.

KCNA imeongeza kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un aliongoza mkutano huo na kuelezea wasiwasi wake kuhusu uharibifu uliofanyika huku akihimiza hatua kali za kurekebisha maeneo yalioathirika.

Kim alikagua maeneo yaliyofurika siku ya Jumapili.

Eneo hilo limeathirika utokana na mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga Gaemi katika siku za hivi karibuni, kilichopelekea maporomoko ya ardhi na kuua watu 12 kusini mwa China na pia kusababisha mafuriko makubwa kwingineko.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii