Walimu wa Shule ya Sekondari Ivumwe inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi iliyopo Kata ya Mwakibete Jiji Mbeya wamefunga geti kwa kutumia gogo wakimzuia Mkuu wa Shule hiyo kuingia ndani mpaka pale watakapolipwa stahiki zao.
walimu pamoja na watumishi wengine wamesema mgomo huo hauna kikomo mpaka pale watakapolipwa stahiki zao ikiwemo mishahara na malimbikizo ya posho.