Afisa mkuu wa Hamas atangaza kusitisha mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza

Afisa wa ngazi ya juu kutoka Hamas, kundi la wanamgambo wa Kiislamu linalochukuliwa kuwa ni kundi la kigaidi na Umoja wa Ulaya, amezungumza Leo siku ya Jumapili kuhusu uamuzi wa kundi hilo la kusitisha mazungumzo ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza, na kushtumu Israel kwa "ukosefu wa umakini" na " mauajiā€.

"Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, Ismail Haniyeh, amewafahamisha wapatanishi na wadau wa kanda katika mfululizo wa wito wa uamuzi wa Hamas wa kusitisha mazungumzo kutokana na kutozingatia uzito wa uvamizi wa Israel (...) na mauaji dhidi ya raia wasio na silaha," mwanachama mkuu wa Hamas amesema.

Siku ya Jumamosi, jeshi la Israel lilithibitisha kwamba lilimlenga mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, Mohammed Deif, katika shambulio lililofanyika kusini mwa Ukanda wa Gaza. Kulingana na Hamas, shambulio hilo lililenga kambi ya watu waliokimbia makazi yao na kuua makumi ya watu.

Afisa huyo mkuu wa Hamas ameliambia shirika la habari la AFP kuwa kiongozi wake wa kijeshi bado yuko hai baada ya shambulizi la Israel.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii