Zelensky amfuta kazi mkuu wa majeshi

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amemfukuza kazi Mkuu wa Majeshi, Valerii Zaluzhnyi, na kumteua Kanali Jenerali Oleksander Syrskyi, aliyekuwa kamanda wa vikosi vya ardhini.


Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov aliyasema hayo siku ya Alkhamis (Februari 8) na kulingana na Zelensky, utawala mpya umeanza kazi mara baada ya uteuzi.

Tangu mwishoni mwa mwaka uliopita, vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti juu ya kutoelewana kati ya Zelensky na Zaluzhnyi.

Siku ya Akkhamis, Zelensky aliandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba amekutana na Zaluzhnyi na kumweleza juu ya hatua hiyo na kujadiliana juu ya mabadiliko yanayohitajika ndani ya jeshi na mtu anayefaa kuchukua nafasi hiyo.

Kulingana na Zelensky, Zaluzhnyi atasalia kwenye timu inayoongoza mapambano dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii