NATO yatafakari kupeleka walinda amani wa kudumu Kosovo na Bosnia

Katibu Mkuu wa NATO, Jumatatu amesema muungano huo unapitia kuongeza moja kwa moja walinda amani wa NATO wa Kosovo na Bosnia wakati huu ambapo kuna ongezeka la ghasia na tahadhari ya uvamizi wa Russia.

Huko Bosnia na Herzegovina, ambapo viongozi wa Bosnia na Serb wameongeza matamshi ya kutaka kujitenga na ushirika huo, katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema kwamba washirika wa NATO wanaunga mkono dola na uhalali wa mipaka yake kwa eneo la Bosnia na Herzegovina.

Stoltenberg, amesema wana wasiwasi na matamshi ya kujitenga na kugawanya, vile vile kuingiliwa vibaya na wageni, ikiwemo na Russia, huko Sarajevo.

Baadaye Jumatatu Stoltenberg, alisimama Kosovo, ambapo Septemba 24 watu wenye na silaha nzito wakiongozwa na mwanasiasa wa Kosovo na Serb, Milan Radojcic, anayedaiwa kuwa uhusiano na rais wa Serbia, Aleksandar Vucic, walishambulia polisi wa Kosovo, na kumuua afisa mmoja.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii