Rais Samia anunua tiketi zote za Mzunguko Taifa Stars Vs Morocco

Rais Samia Suluhu Hassan, amenunua tiketi zote za mzunguko katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar mechi dhidi ya Morocco.


Akizungumza mara baada ya kuwapokea Taifa Stars jana Novemba 19, 2023 wakitokea nchini Morocco walipokipiga na Niger na kupata ushindi wa goli 1-0, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, alisema Watanzania wanatakiwa kujaa uwanjani katika mchezo dhidi ya Morocco utakaopigwa kesho Jumanne.


"Rais ameamua kulipia tiketi zote za mzunguko mechi ya Jumanne" Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa akifikisha taarifa ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania kuelekea mchezo wa Novemba 21, 2023 dhidi ya Morocco wa kufuzu kombe la dunia.


Msigwa pia amekabidhi milioni 10 kwa kikosi Taifa Stars kama hamasa ya #golilamama baada ya ushindi wa jana dhidi ya Niger.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii