• Jumatano , Januari 22 , 2025

Mtibabu bora ya Kinywa, Meno kutiliwa mkazo

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanasimamia matibabu bora ya Kinywa na Meno na kupunguza kung’oa meno bali waongeze watu wanaotibiwa meno.

Ummy ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la 38 la kisayansi la Kitaifa na mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno linalifanyika Jijini Tanga.

Amesema, “Mbali na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri lakini pia Hospitali zote za umma zinazotoa matibabu ya Kinywa na Meno zihakikishe zinaboresha miundombinu ya kliniki za Kinywa na Meno pamoja na kununua vifaa vya kisasa.”

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa, Takwimu za kuziba meno zimeongezeka kutoka asilimia 2 mwaka 2020 mpaka asilimia 36.1 mwaka huu wa 2023 na kusema ipo Mikoa na Wilaya ambayo imevuka asilimia 60.

Hata hivyo amesesitiza kuwa anataka kuona takwimu za kuziba meno zikiendelea kuongezeka na takwimu za kung’oa meno zikipungua na kwamba hali hiyo iende sambamba na utoaji wa elimu ya kinywa na meno kwa ajili ya kuzuia magonjwa yatokanayo na kukosa elimu sahihi ya kujikinga na magonjwa hayo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii