Ridhiwan Kikwete "Jiepusheni na mikopo kausha Damu"

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewatahadharisha Watumishi wa Umma kujiepusha na mikopo yenye riba kubwa maarufu kwa jina la “Kausha Damu” na kusema imekuwa ikidhalilisha utu wa Watumishi katika Jamii.

Kikwete, ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu na kudai kuwa mikopo hiyo imewafanya baadhi ya watumishi wa umma kuathirika kisaikolojia na kushindwa kufika katika vituo vya kazi na hivyo kuathiri utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amesema, Watumishi wanatakiwa kuanza kutumia Mfumo mpya wa kieletroniki wa kukopa (e-loans) ulioanza kutumika kuanzia Septemba 1, 2023 ambao unamuwezesha kuomba mkopo pasipo kufika kwenye Taasisi ya Kifedha, au Tawi la Benki.

Aidha ameongeza kuwa, mfumo huo umeanzishwa na Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora utakaomsaidia Mtumishi wa Umma kupata mikopo katika Taasisi za Kifedha zinazotambulika na Mwajiri, ili kumuepusha kukopa sehemu ambazo humpeleka kunyang’anywa kadi ya Benki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii