Manula is back!

Mlinda Mlango wa Klabu ya Soka ya Simba, Aish Salum Manula ameonekana kuimarika zaidi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Muda Mrefu kutokana na jeraha la lake.


Kipa huyo ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Kocha Robertinho baada ya madaktari kuthibitisha kuwa yupo fiti na anaweza kurejea Uwanjani muda Wowote kuanzia sasa.


Imeelezwa kuwa, Manula amepona kabisa majeraha yake na kilichobaki ni kurejesha fitness yake ili benchi la ufundi waanze kumtumia kwenye mechi za kimashindano.


Manula amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitano akijiuguza baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata mwishoni mwa msimu uliopita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii