Mwimbaji Willy Paul atangaza kuachana na Miss P

Mwimbaji Willy Paul atangaza kuachana na Miss P

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mwimbaji Willy Paul atangaza kuachana na Miss P

Mwanamuziki Wilson Radido almaarufu Willy Paul ametangaza kuwa sasa mahusiano yake na mwenzake Miss P yametamatika, takriban miezi miwili tu baada ya wawili hao kutangaza kuwa wamerudiana.


Katika chapisho kwenye akaunti yake ya Instagram, mwanamuziki huyo akiwahimiza wanawake wanaotaka kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi naye kutuma maombi yao kwake huku akiweka wazi kuwa hayuko kwenye mahusiano na Miss P.


"Ladies, Kwa vile mimi na Miss P Hatupo pamoja tena, nawahimiza sana mtume maombi yenu sasa. Orodha ni ndefu. Kumbuka, muda haumngojei Mwanamke yeyote."


Ndani ya wiki moja iliyopita Willy Paul amekuwa akiashiria kuwa mambo hayako sawa katika mahusiano yake na msanii huyo wake wa kike.


"No pain no gain, angalia hiyo btw nitatoa mature update kuhusu mimi na Miss P. Nikama vitu haziko sawa lakini tunaheshimiana," aliandika Willy Paul wiki jana.


Mnamo Aprili 22, Pozee alimtambulisha Miss P kama mpenzi wake mpya, tangazo ambalo liliwashangaza wanamitandao. Tangazo hili lilikuja baada ya Miss P kuomba msamaha hadharani kwa madai aliyotoa awali kuwa mwanamuziki huyo alikuwa akimbaka.


Mnamo Agosti 2021, Miss P alidai Willy Paul alimnyanyasa kingono mara kwa mara akiwa kwenye studio ya studio ya Saldido.


“Alinilazimisha nifanye naye mapenzi si mara moja si mara mbili, ikabidi nimwambie mama yangu kwa sababu ilibidi nipate huduma ya afya, ikabidi nitafute msaada na mama yangu alinisaidia Alhamdulillah, vinginevyo saa hii ningekua nimesha jifungua au ningekuwa na ujauzito wa miezi tisa," alisema.


Kisha mwaka wa 2023, Miss P aliibuka tena na kukiri kumuharibia jina Pozee. Katika mahojiano na MwanaYouTube Nicholas Kioko, Miss P aliomba msamaha kwa mdai yake ya awali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii