Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress yuko nchini Irak leo kwa mazungumzo na maafisa waandamizi nchini humo baada ya mzozo wa kisiasa kuikumba nchi hiyo.
Ziara hiyo ya Guterres ambayo ni yake ya kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka sita, inakuja wakati ambapo nchi hiyo inayokabiliwa na vita inajiandaa kuadhimisha miaka 20 tangu kuondolewa madarakani kwa dikteta wa muda mrefu Saddam Hussein, katika operesheni iliyoongozwa na Marekani.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesma anataka kuonyesha mshikamano na watu na taasisi za kidemokrasia za Irak na mshikamano unaomaanisha Umoja wa Mataifa umedhamiria kikamilifu kuunga mkono uimarishaji wa taasisi za nchi hiyo.