RASMI CARLO ANCELOTTI KOCHA MPYA BRAZIL

Kocha Carlo Ancelotti amethibitishwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil kwa mujibu wa shirikisho la soka la Brazil (CBF).

Kocha huyo muitaliano ataachana na Real Madrid na atakua kocha wa kwanza mgeni katika timu ya taifa hilo.

Kocha Carlo ameshinda ligi ya mabingwa ulaya mara tano, mara tatu akiwa na klabu ya Real Madrid na mara mbili akiwa na Milan.


Pia ameshinda makombe la ligi na vilabu mbalimbali kama Real Madrid, Chelsea, PSG na Bayern Munich.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii