Ni marufuku kwa maafisa wa Urusi kutumia maneno ya kigeni

Serikali ya Urusi ipo katika hatua ya kuwapiga marufuku maafisa wake kutumia maneno ya kigeni wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria iliyorekebishwa juu ya matumizi rasmi ya lugha ya Kirusi.

Hiyo ni kwa mujibu wa sheria ambayo imefanyia marekebisho na kusainiwa na Rais Vladimir Putin Jumanne iliyopita.

Tangu aanzishe uvamizi wa Ukraine mwaka mmoja uliopita, Rais Putin amesema anataka kuilinda Urusi dhidi ya kile anachokiita uingiliwaji wa mataifa ya Magharibi ambayo anayatuhumu kuvuruga taifa lake.

Hata hivyo mabadiliko hayo ya sheria ya mwaka 2005 hayaoneshi adhabu yoyote kwa atakekutwa na hatia ya kuikiuka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii