Kamishna Mkuu Wa KRA, Mburu Ajiuzulu

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru ya Kenya (KRA) Bw Githii Mburu, alijiuzulu jana, mwaka mmoja kabla ya muhula wake kukamilika.

Bodi ya KRA ilisema kwamba Bw Mburu alijiuzulu kushughulika na masuala ya kibinafsi na ikamteua Bi Rispah Simiyu kuchukua nafasi yake kwa muda huku ikisaka kamishna mkuu mpya.

“Kufuatia kujiuzulu kwake, bodi imemteua Rispah Simiyu (EBS), kama kaimu Kamishna Mkuu wa KRA kuanzia Februari 23, 2023 hadi nafasi hiyo itakapojazwa,” KRA ilisema kwenye taarifa.

Bw Mburu aliteuliwa mwaka wa 2019 na Rais Uhuru Kenyatta kwa muhula wa miaka mitano ambao ungekamilika Juni 2024

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii