Polepole"Watanzania changamkieni fursa Malawi "

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Humfrey Polepole amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo nchini Malawi, huku akiahidi Ubalozi huo utaendelea kuwasaidia kupata masoko sahihi.


Akizungumza Balozi Polepole amebainisha kuwa kwa kiasi kikubwa wananchi wa kipato cha chini na kipato cha kati wanategemea zaidi bidhaa kutoka Tanzania.

Aidha Balozi Polepole akatoa ufafanuzi kuhusu changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo madereva wa malori wakiwa nchini Malawi, akiwataka kutosita kumpigia ikiwa watapata changamoto yoyote wakiwa njiani.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii