Mzee Luhende Tugwa (80) mkazi wa Kijiji cha Ihapa Kata ya Old Shinyanga anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake anayesoma shule ya msingi Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga (jina limehifadhiwa) baada ya kutoka shule.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amethibitisha kutokea tukio hilo ambapo amesema lilitokea jana mchana baada ya mwanafunzi huyo kutoka shule na kurejea nyumbani na kumkuta babu yake huku bibi yake akiwa ameenda shambani ndipo mtuhumiwa aliamua kutumia fursa hiyo kufanya kitendo hicho cha ukatili kwa mtoto
Kamanda Janeth amesema kuwa wanamshikilia mzee huyo kwa hatua zaidi za kisheria ili kujibu tuhuma zinazomkabili,huku akiitaka jamii kuendelea kukemea vitendo vya ukatili na kuwafichuwa watu wanaoendelea kufanya ukatili kwa wanawake na watoto