Dawati la Jinsia Nchini Lajipanga Kutoa Elimu ya Afya ya Akili

MKUU wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna, Mary Nzuki amewataka Askari Polisi wanaofanya kazi Dawati la Usalama Wetu kwanza kuwapa elimu ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia Watoto ambao ni wahanga wa vitendo vya ukatili.

 

Ametoa kauli hiyo Septemba 19, 2022 wakati akifungua mafunzo ya siku saba yq kuwajengea uwezo wa afya ya akili na msaada wa kisaikolojia jijini Dar es Salaam kwa Askari Polisi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambapo amesema kuwa elimu na msaada huo unatakiwa kutolewa mashuleni na nyumbani kwa kushirikiana na wazazi, walimu na wadau wenye dhamana ya malezi ya watoto.

 

Aidha naibu kamishina wa Polisi ambae pia ni mkuu wa Dawati la jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Nchini DCP- Mary Nzuki  alisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kiutendaji Askari katika utoaji elimu kwa watoto Pamoja na shule wanazozifundisha ili wasijiingize kwenye vitendo vya kihalifu pamoja na kutoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto wahanga wa vitendo vya ukatili.

 

Pia amewataka washiriki kuwa makini na elimu watakayoipata iwe na ufanisi na kuleta tija kwa Watoto walioko ndani ya jamii. Ambapo mkurugenzi Mkaazi wa Asasi y REPSSI Bw EDWICK GAMANYA MAPALALA alisema kumekuwa na matukio mengi ya visasi na vifo yanayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo msongo wa mawazo na afya ya akili hivyo mafunzo hayo yataleta tija kwa askari Polisi namna ya kushughulikia kesi na kutoa elimu wa watoto kupitia madawati yao.

 

Amebainisha kuwa Taasisi hizo zimeona ni vyema kushirikiana na Jeshi Polisi kutoa mafunzo hayo kuhakikisha kunakuwa na usalama wa watu kiakili kwani kuna changamoto kuanzia ngazi ya familia, hadi katika kijamii.

Ameongeza kuwa kutokana na changamoto hizo, wameo ni vyema kuwaongeza kuwa ujuzi na watakao upata utamwezesha kila askari kuupelekea Wananchi hususani kuwalinda na kuwapa upendo makundi maalum likiwemo la Watoto ambao ni waanga wakubwa wa matukio ya ukatilii.

 

Ufunguzi wa mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Asasi za REPSSI Tanzania kwa kushirikiana na SOS Children’s Villages na (The Families and Future Coalition of Tanzania (FFCT) ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Dkt. Lazaro Mambosasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii