Katibu Mkuu wa UN kukutana na viongozi wa Ukraine, Uturuki mjini Lviv

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atakutana na viongozi wa Ukraine na Uturuki kesho, ili kutathmini utekelezaji wa mkataba ulioruhusu kuanza kusafirishwa tena kwa nafaka ya Ukraine, pamoja na njia za kidiplomasia za kukomesha vita Ukraine. Guterres atafanya mazungumzo katika mji wa magharibi mwa Ukraine wa Lviv na Rais Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema watajadili kuhusu suluhisho la kisiasa kwa mzozo unaoendelea. Guterres kisha atazuru mji wa bandari wa Odessa nchini Ukraine siku ya Ijumaa - ambayo ni mojawapo ya bandari tatu zinazotumika kusafirisha nafaka, kabla ya kuelekea Uturuki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii