Kiongozi mkuu mpya wa kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV ameongoza ibada ya kwanza ya misa takatifu ikiwa ni siku moja tu, iliyoleta furaha kwa waamini wengi wa kanisa katoliki na Mmarekani wa kwanza kuliongoza kanisa hilo lenye wafuasi wengi duniani.
Ikumbukwe kuwa Papa Leo XIV ni mzaliwa wa Chicago ambapo kabla ya kuwa Papa alikuwa akitambulika zaidi kwa jina lake la Robert Francis Prevost na alichaguliwa jana Alhamisi kuwa papa wa 267, hata hivyo kiongozi huyo wa kiroho mwenye waumini wengi duniani takribani bilioni 1.4 wa kanisa Katoliki ndiye anachukua nafasi kwa sasa kuliongoza kanisa hilo, kufuatia mkutano maalumu wa makadinali wenzake katika makazi rasmi ya Papa kanisa la Sistine mjini Vatican.
Papa huyo mwenye umri wa miaka 69, amerejea katika kanisa hilo kuongoza misa ya faragha na makadilani iliyooneshwa moja kwa moja na makao makuu Vatican, akitoa hotuba yake ya kwanza kama Papa iliyosubiriwa na waamini wengi wa imani hiyo.