Mhasibu Wizara ya Mambo ya Ndani ahukumiwa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Mhasibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini, Christina Kaale kulipa faini ya Sh8 milioni au kwenda jela miaka miwili, baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa Sh15.2 milioni mali ya wizara hiyo.

Kaale anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya sherehe ya kuwaaga wafanyakazi wastaafu wa wizara hiyo.

Pamoja na adhabu hiyo, mahakama pia imemtaka Christina kuilipa fidia Wizara hiyo ya Sh15.2 milioni anazodaiwa kufanya ubadhirifu, mara atakapomaliza kutumikia adhabu kifungo.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Julai 29, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii