Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amejumuishwa kwenye kikosi kazi kinachoendelea na shughuli ya kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa.
Pinda aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya awamu ya nne, amejukuishwa leo Jumatatu Mei 302022 kwenye Kikosi hicho kilichoteuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ikiwa mwezi mmoja sasa umepita tangu kuanza shughuli ya kukusanya maoni hayo.
Msajili wa Vyama vya Siasa alimtambulisha rasmi Pinda mbele ya wajumbe wengine wanaounda kikosi tayari kwa kuendeleza shughuli.
Katika kikao hicho cha kumtambulisha kiliongozwa na Jaji Mutungi na baada ya mazungumzo ya kumtambulisha kiongozi huyo ilikuja Coaster nyeupe kumchukua akiambatana na baadhi ya viongozi akiwamo Profesa Rwekaza Mkandara ambaye ni mwenyekiti wa kikosi hicho.
Kwa mujibu wa mjumbe mmoja ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema kiongozi huyo amekuja kuongeza nguvu katika kikosi hicho.
"Amekuja kutambulishwa leo rasmi na tutakuwa naye hadi mwisho wa kukusanya maoni na kama umemuona anatoka hapa na baadhi ya wajumbe wameenda kuonana na Rais Ikulu," amesema
Amesema kikosi hicho kuna wakati huwa kinaelemewa na hoja za wanaokuja kutoka maoni hivyo wanaamini uwepo wake na uzoefu wake watasaidia kuongeza utulivu.