Raia wa Colombia wanapiga kura leo katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, huku chama cha mrengo wa kushoto kikielekea kuibuka na ushindi kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo ya Amerika Kusini.Uchaguzi huo unafanyika katika hali ya wasiwasi, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu ukandamizaji mkali ya vikosi vya usalama dhidi ya maandamano ya mitaani ambayo yalichochewa na kuongezeka kwa matatizo ya kijamii na kiuchumi.Kura za maoni zinaonyesha kwamba wananchi wengi wa Colombia wanaweka matumaini yao kwa Gustavo Petro, mpiganaji wa zamani na meya wa zamani wa Bogota, ambaye anabeba matumaini ya kushughulikia umaskini, machafuko, uhalifu wa mijini na ufisadi uliokithiri.Takriban polisi 300,000 wenye silaha na wanajeshi wamesambazwa katika vituo 12,000 vya kupigia kura nchini kote kwa lengo la kulinda amani. Waangalizi wa uchaguzi kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya wanafuatilia uchaguzi huo.