Katibu
Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, amewaonya viongozi waliopewa dhamana na
chama hicho, kuacha kueneza fitina na majungu dhidi ya wengine wakati wa
uchaguzi wa ndani.
Chongolo ameyasema hayo leo Mei 27, 2022
wakati akisalimia wanachama wa CCM Mkoa wa Shinyanga, alipofika kwa
ajili ya ziara ya kikazi.
Mtendaji Mkuu huyo wa CCM, amesema chama hicho kina utaratibu, Katiba, Kanuni na miongozo iliyondaliwa vizuri.
Amewataka
kutenda haki, akieleza kuwa haiwezekani wakati wote tangu mwaka 2017
viongozi hao wamekuwa ndani ya CCM lakini hawakuwahi kuonywa wala
kujadiliwa kwenye vikao vya maadili, iweje tuhuma hizo ziibuke sasa.