Odinga kumtangaza mgombea mwenza

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, anatarajiwa kumtaja mgombea mwenza hii leo, baada ya kupokea majina matatu kutoka kwa jopo alililoteuwa kumsaidia kumchagua mgombea mwenza.

Majina matatu aliyopokea Odinga ni pamoja na aliyekuwa makamo rais Kalonzo Musyoka, ambaye pia amekuwa mgombea mwenza katika chaguzi mbili zilizopita, wengine ni aliyekua mbunge na waziri Martha Karua na Peter Kenneth.

Tume ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC ilitangaza leo kuwa siku ya mwisho kwa  wanaogombea urais kuwasilisha majina ya wagombea wenza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.

Odinga mwanasiasa wa upinzani wa muda mrefu nchini Kenya, anaungwa mkono na rais Uhuru Kenyatta kuwa mrithi wake, baada ya uhusiano wa Kenyatta na naibu wake William Ruto, kuyumba kwa kipindi cha minne iliopita.

Katika hatua nyingine mpinzani mkuu wa Odinga, katika uchaguzi wa agosti nane, naibu  rais william Ruto, amemteua mbunge wa Mathira, Rigathi Gachaugua kuwa mgombea mwenza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii