Wagombea 36 kushiriki katika uchaguzi wa rais nchini Somalia hii leo

Wagombea 36 wanawania kiti cha rais katika uchaguzi unaofanyika leo nchini Somalia ambao umecheleweshwa kwa muda mrefu.Rais huyo atachaguliwa na wabunge katika eneo la uwanja wa ndege lililo chini ya ulinzi mkali katika mfumo ambao hauwashirikishi wananchi wote.Marais wawili wa zamani na kiongozi mmoja wa kikanda pia wanawania wadhifa huo. Ni mwanamke mmoja tu aliyejitokeza kushiriki katika kinyang'anyiro hicho. Wawakilishi 275 wa bunge na maseneta 54 watamchagua rais huyo katika duru kadhaa za uchaguzi. Kamati ya maandalizi ya bunge imekitaka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika kulinda eneo hilo la uwanja wa ndege mjini Mogadishu. Mwezi uliopita, walinzi hao walikabiliana na wakazi wa eneo hilo wakati wa uchaguzi wa spika wa mabunge hayo mawili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii