Mahakama ya Pakistan yaamuru uchunguzi kuhusu kukamatwa kwa waziri wa zamani

Mahakama Kuu ya mji mkuu wa Pakistan, Islamabad imeamuru uchunguzi ufanyike juu ya kitendo chenye utata cha kukamatwa kwa aliyekuwa waziri wa haki za binadamu wa nchi hiyo Shireen Mazari kwa tuhuma za mgogoro wa zamani wa ardhi. Jaji Mkuu Ather Minallah wa Mahakama Kuu ya Islamabad ameamuru uchunguzi huo na kusema anatilia shaka uamuzi wa mamlaka kuwaruhusu polisi wa wilaya ya mkoa wa Punjab kumkamata kiongozi huyo wa zamani. Mazari ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya sasa, alihudumu katika utawala wa aliyekuwa waziri mkuu Imran khan, na chama chake kimekuwa kikilengwa kisiasa na utawala mpya wa waziri mkuu Shahbaz Sharif kwa kivuli cha mgogoro wa ardhi ulioanza mwaka 1972.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii