Rais mteule wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, anasema serikali yake italenga masuala ya haraka ikiwa ni pamoja na usalama, kufufua uchumi, uthabiti wa kisiasa, na auheni ya madeni katika kipindi chake cha siku 100 za kwanza madarakani.
Mohamud alichaguliwa Jumapili kwa mara ya pili, akimshinda kiongozi aliyepo madarakani Mohamed Abdullahi Mohamed. Mohamud anarejea madarakani baada ya kuhudumu kama rais kutoka mwaka 2012 hadi mwaka 2017.
“Tunataka kutekeleza kile tunachotaka kufanya katika siku zangu 100
za kwanza ofisini. Tunataka kufanya mageuzi ya mfumo wa zamani wa
kisheria na muundo wa mashirika yetu ya usalama, tunataka kuvishirikisha
vyombo vya usalama” Mohamed alisema
Kupambana na al-Shabaab kundi la kigaidi lenye uhusiano na al-Qaida ambalo limeongeza mashambulizi yake mjini Mogadishu katika miezi ya karibuni ni moja ya changamoto kubwa sana zinazomkabili rais huyo.