WATALIBANI WATANGAZA KUSITISHA MAPIGANO.

Wataliban wa Pakistan wamesema wataendeleza muda wa kusimamisha mapigano na serikali ya Pakistan hadi mwishoni mwa mwezi huu. Wajumbe wa pande hizo mbili walikutana chini ya unyekiti wa serikali ya Taliban ya nchini Afghanistan. Serikali hiyo imethibitisha kwamba hatua ya kusimamisha mapigano imefikiwa kati ya Taliban wa Pakistan na serikali ya nchi hiyo. Msemaji wa kundi hilo la Taliban nchini Pakistan Mohammad Khurasani,ameeleza kuwa wanafanya kila juhudi ili mazungumzo yasonge mbele. Wataliban wa Pakistan wanataka sheria kali za kiislamu ziendelezwe na pia wanataka wapiganaji wao waliokamatwa waachiwe.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii