Kura za mapema zaanza kupigwa Australia

Upigaji kura wa mapema umeanza nchini Australia leo, wiki mbili kabla siku ya kupiga kura, huku matokeo ya utafiti wa maoni yakionesha chama cha upinzani cha Labour kikiongoza na waziri mkuu Scott Morrison akipata pigo katika umaarufu wake. Utafiti wa maoni uliofanywa na gazeti la Australian umeonesha chama cha Labour kinaongoza kwa asilimia 54 kwa 46 dhidi ya serikali ya mseto inayokijumuisha chama cha kiliberali na chama cha kizalendo. Umaarufu wa Morrison umeshuka hadi asilimia 44 akiwa mbele ya kiongozi wa upinzani Anthony Albanese ambaye umaarufu wake umeongezeka kwa alama tatu hadi asilimia 42. Upigaji kura wa mapema umeanza siku moja baada ya mdahalo wa televisheni kati ya Morrison na Albanese ambapo mara kadhaa walipigiana kelele kiasi cha mahasimu hao kushindwa kuwasilisha hoja zao vizuri.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii