Wabunge wa Somalia waapa

Wabunge wa Somalia wamekula kiapo chao kuanza kazi ikiwa ni hatua muhimu kulekea katika uchaguzi wa kiongozi mpya wa taifa hilo, hatua ambayo imekuwa ikicheleweshwa kwa miezi kadhaa iliyogubikwa mzozo wa kimamlaka kati ya rais wa sasa na waziri mkuu wake. Siku ya Alhamis, wabunge 250 katika ya 275 ambao wanateuliwa na viongozi wa kikoo, walikula viapo vyao pamoja na maseneta 40 kati ya 50 chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya jeshi la Umoja wa Afrika mjini Mogadishu.Uchaguzi ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka mmoja uliopita lakini ulicheleweshwa kutokana na Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kufanya jaribio la kurefusha muhula wake wa miama minne kwa kuongeza miwili ya ziada hatua ambayo ilizuiwa na bunge.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii