Maafisa wa zamani wa chama kilichopigwa marufuku PKK wakamatwa nchini Uturuki

Mamlaka nchini Uturuki zimewakamata na kuwashikilia watu 46 wakiwemo maafisa wa zamani wa chama cha kisiasa kinachounga mkono harakati za wakurdi-PKK,ambao wanashukiwa kuwa na mafungamano ya kuwasaidia kifedha wanamgambo wa kikurdi. Hayo yameripotiwa na shirika la habari linaloendeshwa na serikali. Waliokamatwa ni miongoni wa washukiwa 91 wanaotafutwa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kwa madai ya kuwa vyanzo vya fedha vya kusaidia harakati kwa niaba ya chama hicho kinachojulikana kama chama cha wafanyakazi wakurdistan PKK ambacho kimepigwa marufuku nchini Uturuki. Wanatuhumiwa kuwa sehemu ya mfumo wa kiuchumi wa chama hicho unaodaiwa kuhusika na utakatishaji fedha na kupokea maagizo kutoka kwa kamanda wake Murat Karayilan.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii