Covid yaongeza hatari kwa walioambukizwa kuganda damu

Utafiti uliochapishwa leo umeonyesha kuwa watu waliaoambukizwa virusi vya corona wako hatarini kupata tatizo la kuganda damu hadi miezi sita baada ya kuambukizwa. Utafiti huo umegundua kwamba watu waliopata maambukizi makali ya covid na wenye maradhi sugu wako hatarini zaidi ingawa hata waliopata maambukizi yasiyo makali pia wametajwa kuwa hatarini kupata tatizo hilo. Kufuatia utafiti huo wataalamu hao wanatoa mwito wa matibabu zaidi ya kuzuia kuganda kwa damu na hasa kwa wagonjwa walio hatarini zaidi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii