Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema jana kwamba dharura za kiafya zinazosababishwa na mazingira zinaongezeka barani Afrika ingawa linachangia kidogo mno ongezeko la joto ulimwenguni. Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dr. Matshisido Moeti amesema uchambuzi wa WHO umeonyesha zaidi ya nusu ya visa vya dharura vinavyohusiana na matatizo ya kiafya kwa umma vimerekodiwa barani humo katika kipindi cha miongo mwili iliyopita. Amesema mafuriko ya mara kwa mara yanasababisha magonjwa yanayoambukizwa kwa maji na kuongeza mizozo ya kiafya barani humo ingawa mchango wake kwenye mabadiliko ya hali ya hewa ni mdogo mno. Asilimia 56 ya visa hivyo vilivyorekodiwa kati ya mwaka 2001 hadi 2021 vilihusiana na mabadiliko ya hali ya hewa