Wanasayansi wa UN wahimiza kuachana na nishati chafu ili kuiokoa dunia

Wanasayansi wa Umoja wa Mataifa wamesema malengo yaliyowekwa na jumuiya ya kimataifa ya kudhibiti ongezeko la joto duniani katika kiwango cha nyuzi 1.5 za Celsius yatatekezeka tu ikiwa itafanyika mipango kabambe ya kusitisha utoaji wa gesi ya ukaa. Mkuu wa jopo la wataalamu hao, Hoesung Lee amesema dunia iko njiapanda, lakini maamuzi yanayochukuliwa leo yanaweza kuweka mazingira ya dunia nzuri kwa maisha ya watu siku za usoni. Tathmini ya mwaka huu ya kikundi hicho cha wanasayansi ilijikita katika namna mabadiliko ya tabianchi yatokanayo na shughuli za binadamu yanavyoweza kudhibitiwa. Uchunguzi wao unaonyesha kuwa ikiwa hakuna mabadiliko yatakayofanyika katika mtindo wa maisha wa binadamu wa sasa,mnamo miaka michache ijayo malengo ya kudhibiti ongezeko la joto katika nyuzi 1.5 yatageuka ndoto isiyowezekana kutimizwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii