Mshambuliaji kutoka nchini Niger na klabu ya USGN Victorien Adebayor amesema mchezo dhidi ya Simba SC hakuwa na changamoto kubwa sana kwa upande wake, licha ya baadhi ya Mashabiki kuona alikua kwenye hali ngumu.
Adebayor ambaye alikua msaada mkubwa kwa USGN tangu walipopanza michuano ya kimataifa msimu huu 2021/22, amesema Simba SC ni klabu kubwa Barani Afrika na alilitambua hilo, hivyo alijiandaa kisaikolojia na alifanikiwa.
Amesema kuna wakati hakutaka kupambana kwa nguvu kwa sababu alijua
Simba SC wanamtazama kama adui katika lango lao, hivyo alipambana
kawaida na ndio maana alipokua akipata nafasi alizitumia kwa umakini
japo hakufanikiwa.
“Ulikua mchezo mgumu sana, lakini kwangu
nilijiandaa kwa kila hali kwa sababu nilijua isingekua rahisi, nashukuru
hilo lilifanikiwa licha ya mambo kutuendea vibaya hadi mwishoni mwa
dakika 90.”
“Sikuwa na Presha kabisa, kwa sababu nimewahi kucheza michezo migumu zaidi ya tulivyocheza hapa na Simba SC, nilijitahidi kwa kushirikiana na wenzangu na nilijaribu kutumia nafasi nilizozipata lakini sikufanikiwa na wala timu haikufanikiwa.” amesema Adebayor alipozungumza na Jembe FM.