Macky Sall atoa wito kwa raia kukabiliana na kupanda kwa bei za vyakula

Rais wa Senegal alilihutubia taifa katika mkesha wa kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa nchi hiyo. Wakati Waislamu wakianza mfungo wa Ramadhani Jumapili hii, Aprili 3 na Wakristo wakiwa katikati mfungo wa Kwaresima, Rias Macky Sall alisisitiza juu ya masuala ya bei ya vyakula na kujitosheleza kwa chakula.


Baada ya miaka miwili bila sherehe kwa sababu ya janga la Covid-19, sherehe ya kuchukua silaha ikifuatiwa na gwaride la kijeshi litakalo kuwa na "idadi ndogo ya wanajeshi" katika Uwanja wa Uhuru itaadhimisha kumbukumbu ya miaka 62 ya huru wa Senegal Jumatatu hii, Aprili 4. Lakini hotuba ya Rais Macky Sall ilikuwa juu ya yote wito wa maandamano, katika muktadha wa kupanda kwa bei kunakohusishwa na vita vya Ukraine.

“Kwa kuzingatia hatari kubwa ya uhaba na kupanda kwa bei kutokana na msukosuko wa dunia, naomba uhamasishwaji wa ujumla ili kuongeza na kuimarisha zaidi mazao yetu ya kilimo, mifugo na uvuvi,” alisema.

"Kukabiliana na changamoto ya kujitosheleza kwa chakula"

Rais wa Senegal pia alieleza kwa undani jinsi ya kupunguza bei za mahitaji ya kimsingi na kuongeza ruzuku ya mchele wa ndani kusaidia kaya mbalimbali. "Lakini ili kulindwa kutokana na hali duni ya hali ya kimataifa, lazima tuonyeshe uthabiti kwa kushinda vita vya uhuru wa chakula haraka iwezekanavyo. Huu ni uwekezaji mkubwa ambao serikali inaendelea kujitolea katika uboreshaji wa kisasa na mseto wa sekta ya mifugo, uvuvi na kilimo. Kukabiliana na changamoto ya kujitosheleza kwa chakula pia hurahisisha biashara kati ya maeneo ya uzalishaji na masoko. "

Wakati kaulimbiu ya siku hii ya uhuru ni vikosi vya ulinzi na usalama na uimara wa taifa, Macky Sall pia alisisitiza kuendelea kwa "mpango wa kujenga uwezo wa jeshi" ili kuwa tayari kuhakikisha ulinzi wa taifa "katika hali ya misukosuko." na muktadha wa kimataifa usio na uhakika. "

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii