Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin amesema wachezaji wake wamekamilisha Program ya maandalizi kabla ya kuikabili USGN leo Jumapili (April 03) saa nne usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Simba SC kilifanya mazoezi ya mwisho jana Jumamosi (April 02) Usiku, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambako mchezo dhidi ya USGN utapigwa leo Jumapili (April 03).
Kocha Pablo amesema wachezaji wake wamepata muda mzuri wa kujiandaa na mchezo huo, na Uongozi umefanya kazi yake ipasavyo kwa kumtimizia mahitaji yote aliyoyawasilisha juma moja kabla ya kuanza kambi.
Amesema kwa misingi hiyo anaamini wachezaji wake watapambana kwa kutumia mbinu alizowafundisha karibu juma zima, hivyo amewataka mashabiki kuendelea kuwa na imani na kikosi chao kitakachoikabili USGN baadae leo Jumapili (April 03).