Bunge la Pakistan kuanza kujadili hoja ya kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Khan

Bunge la Pakistan leo litaanza mjadala wa kutokuwa na imani na uongozi wa Waziri Mkuu Imran Khan. Hatua hii huenda ikapelekea kuondolewa madarakani kwa mchezaji huyo wa zamani wa kriketi na nchi hiyo iliyojihami na silaha za nyuklia kurudi katika swintofahamu ya kisiasa. Hapo jana, chama rafiki kwa waziri huyo mkuu Muttahida Qaumi Movement MQM, kilijiondoa kutoka kwenye muungano wake na kuunga mkono upinzani unaotaka kumuondoa mamlakani. Kura kuhusiana na mswada wa kumuondoa madarakani Khan inatarajiwa kupigwa ifikiapo Jumatatu. Uongozi wa Khan mwenye umri wa miaka 69 umekosolewa pakubwa ikiwemo jinsi alivyosimamia uchumi unaokabiliwa na mfumko mkubwa wa bei na madeni yanayoongezeka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii