Wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM wamemchagua Abdulrahman Kinana kuwa makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa kura za ndiyo 1875.
Wajumbe waliopiga kura 1875, jura halali 1875, hakuna za hapana wala zilizoharibila
Matokeo hayo yametangazwa leo Ijumaa Aprili 1, 2022 na Dk Tulia Akson ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Abdulrahman Kinana amepanda kukaa meza kuu kwenye nafasi yake huku mtangulizi wake Philip Mangula akikiachia rasmi kiti hicho na kumpisha.
Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesoma barua ya kumg’atuka kwa makamu mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula leo Ijumaa Aprili 1, 2022 mbele ya Mkutano Mkuu unaoendelea mjini Dodoma.