Afrika Kusini yarekodi vifo 100,000 vya COVID-19

Afrika Kusini imerekodi zaidi ya vifo 100,000 vya virusi vya corona. Kwa mujibu wa takwimu za serikali zilizochapishwa jana, vifo 100,020 vimetokea tangu janga hilo lilipoanza miaka miwili iliyopita. Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Afrika Kusini jana ilirekodi vifo 44, lakini vifo sita tu vilirekodiwa siku mbili zilizopita. Taasisi hiyo imesema vifo vingine viligunduliwa wakati wa ukaguzi wa serikali unaoendelea. Kwa upande wake Marekani imesema watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 11 ambao wamepata chanjo ya virusi vya corona ya BionTech/Pfizer walikuwa na uwezekano mdogo za kulazwa hospitali wakati wa wimbi la kirusi aina ya Omicron nchini humo, kwa asilimia 68 kuliko ambao hawajachanjwa. Nayo taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza nchini Ujerumani, Robert Koch leo imerekodi visa vipya 274,901 na vifo 279 vya maambuizi ya virusi vya corona.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii