WFP: Vita ya Ukraine yavuruga mipango ya chakula

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP David Beasley ameonya kuwa vita vya Ukraine vinatishia kuvuruga juhudi za shirika hilo kuwalisha takribani watu milioni 125 duniani kote kwa sababu Ukraine imetoka kuwa mlimaji wa nafaka ulimwenguni na kuwa kwenye foleni ya watu wanaosubiri msaada wa chakula. Beasley ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba asilimia 50 ya nafaka inayonunuliwa na WFP inatoka Ukraine, hivyo ni wazi mipango ya shirika hilo inavurugika. Amesema vita hivyo, haviiangamizi tu Ukraine na eneo hilo, bali pia vina athari kwa muktadha wa kimataifa ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Amesema mzozo huo umechangiwa na ukosefu wa bidhaa za mbolea zinazotoka Belarus na Urusi na kuonya iwapo hautomalizika, dunia itashuhudia WFP ikichukua chakula kutoka kwa watoto wanaohitaji chakula na kuwapa watoto wanaokufa kwa njaa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii