Dkt. Mabula ataka elimu itolewe ugawaji wa ardhi

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametaka elimu ya kuwatahadharisha wananchi kuhusu kujiepusha na vishawishi visivyo na tija vinavyosababisha ugawaji maeneo ya ardhi kwa ajili ya uwekezaj kwa kupewa ahadi zisizotekelezeka.

Dkt Mabula amesema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha Wadau wa Uandaaji, Usimamizi na Utekelezaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma.

‘’Tunategemea ninyi wadau mnakuwa sehemu ya kuelimisha wananchi kutambua thamani ya ardhi na kutokuwa wepesi kuachia ardhi kwa sababu ya tamaa ya wawekezaji, wanakuja halafu wanakuwa ahadi isiyotekelezeka na mwisho wa siku wananchi wanapeleka kilio serikalini’’ amesemaDkt. Mabula

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii