Timu ya taifa ya Senegal, imefuzu kushiriki katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika baadae mwaka huu huko Qatar. Senegal mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2021, imefuzu baada ya kuifunga Misri kwa mikwaju ya penati 3 kwa 1. Timu hiyo ilikuwa ikimtegemea nyota wake Sadio Mane kuivusha, ambaye hakufanya kosa na kuipatia ushindi. Senegal sasa itaungana na timu nyingine za Afrika; Ghana, Tunisia, Cameroon na Morocco. Ghana imefuzu baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1 kwa 1 na Nigeria, na kupata faida ya bao la ugenini. Tunisia imefanikiwa licha ya kutoka sare ya bila kufungana na Mali katika mchezo wa jana, hivyo imefuzu kwa bao 1 kwa bila ushindi wa jumla. Cameroon imefuzu kwa kuifunga Algeria mabao 2 kwa 1. Morocco imefuzu kwa kuifunga Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mabao 4 kwa 1.