Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro
linamshikilia Abdilah Yassin mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro
mpigadebe katika kituo kikuu cha mabasi cha Msamvu mkoani Morogoro kwa
kusababisha mauaji kwa kumchoma kisu mpigadebe mwenzie Tazani Mndeme
mkazi wa Mwembesongo wakigombea abiria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa
Jeshi la Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo.
Amesema katika ugomvi huo wa kugombea abiria Abdilah
Yassin ambaye anafika zaidi kwa jina la “HAJIMONGA BONGE” alimchoma kisu
kifuani upande wa kushoto Tazani Mndeme ambapo alikimbizwa hospitali ya
Rufaa Mkoa wa Morogoro na kufariki wakati akipatiwa matibabu
hospitalini hapo.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii