Mtandao Wawaka Moto Baada ya Rais Kusema DP Ruto Alitaka Kumng'oa Mamlakani

Mtandao wa kijamii wa twitter Jumapili Machi 27 asubuhi uliwaka moto baada ya ripoti za mazungumzo ya Rais Uhuru Kenyatta na wazee kutoka Mt Kenya.
Rais alifanya kikao hicho Jumamosi Machi 26 na jarida la Standard Jumapili likachapisha yaliyosemwa.
Mojawapo wa hoja za Rais kwa wazee hao ilikuwa ripoti kuwa naibu wake William Ruto alikuwa amepanga kumng'atua mamlakani .
Ni taarifa ambayo imeibua hisia mseto kwenye twitter huku wakosoaji wa Rais wakigeuka watani.
Baadhi walisema hulka za Rais zimekuwa kama za mvulana mdogo anayetafuta huruma kutoka kwa wazazi mambo yakimwendea mrama.kani.
"Uhuru anafikiria akiambia Wakikuyu eti Ruto alikuwa amejaribu kumng'atua watamhurumia na kuhisi woishe, woiye ama pole kababa, na kisha kufana tumchukie Ruto na kumpigia kura Raila," Mumbi Mbui aliandika

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii