Mahakama ya Afrika Mashariki kuamua kesi ya vyama vya siasa leo

Majaji watano wa Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) leo Ijumaa Machi 25, 2022 wanatarajia kutoa uamuzi wa kesi namba 3 ya mwaka 2019 iliyofunguliwa na vyama vitano vya siasa na kesi namba 4 ya mwaka 2019 iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya kupinga vifungu vya sheria ya vyama vya siasa.

Viongozi wa vyama vya siasa wakiongozwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe tayari wapo mahakamani hapa pamoja na mawakili wa LHRC kusubiri maamuzi haya.

Katika kesi hizo mbili zilifunguliwa kwa nyakati tofauti, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliomba mahakama hiyo kuziunganisha kuwa kesi moja kwa kuwa hoja za walalamikaji zinalenga jambo moja la kupinga Sheria ya Vyama vya Siasa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Katika kesi hiyo, LHRC inadai mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019 yanakiuka mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao Tanzania iliridhia na kuwa miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 20 iliyopita.

 LHRC inadai sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano, Januari 29, 2019 kusainiwa na Rais na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali Februari 22, 2019 ina upungufu mwingi ambayo inaiomba EACJ iyabatilishe.

Katika kesi hiyo ambayo imefanyika kwa njia ya mtandao LHRC inadai mkataba ulioanzisha EAC ibara ya 4,6(d),7(2),8(1)(c),27(1),30(1) na 38(2) pamoja na kanuni za mahakama hiyo ibara ya 1(2) na 24 ya mwaka 2013 zimekiukwa pia inadai mabadiliko ya sheria y

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii