Ujerumani yasaidia kukabiliana na kitisho cha njaa Ukraine

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema taifa lake litaunga mkono utoaji wa misaada ya kiutu kwa Ukraine na mataifa jirani kwa kutoa nyongeza ya Euro milioni 370, kadhalika nyongeza ya Euro 430 kwa kukabiliana na kitisho cha njaa.Akizungumza baada ya mkutano wa kundi la mataifa saba yenye nguvu ya uchumi wa kiviwanda duniani, yaani G7 na ule wa viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, ametoa wito kwa mataifa mengine kutoa misaada zaidi. Amesema vita vya Urusi vimekuwa na athari kubwa katika usambazaji wa vyakula hata nje ya mipaka ya Ukraine. Kwa hivyo lazima kuwe na jitihada za makusudi kukabiliana baa la njaa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii